Mzee wa Siku ni Wimbo ambao ulitungwa rasmi na kuimbwa Mwaka 2009 ukibeba jina la Albam ya Pili baada ya Majaribu ni Mtaji. Albam hiyo ilijulikana Kama Mzee wa Siku au Heshima ya Mrefu ni Mfupi ikiwa na nyimbo za kuinua moyo na kutia nguvu Mwamini kuyashinda Majaribu na changamoto za maisha.

Mwaka 2023 nilifanikiwa kufanya ibada ya Shukrani ya miaka 20 ya huduma Mlimani City na Mungu alinipa nafasi ya kuimba live wimbo huu siku hiyo.

Na hii ndiyo ibada na video yake Ilivyokuwa.

Karibu sana ubarikiwe na wimbo huu kwa Mara nyingine na Mungu mwenyewe akuhudumie kwa jina la Yesu. Amen